Habari

Mwenyekiti awanunulia wananchi filimbi ili kujihami na matukio ya kihalifu

Baada ya matukio ya kutisha kutokea mara kwa mara katika mtaa wa Utemini kata ya Mkolani Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza, mwenyekiti wa mtaa huo, Jukaeli Kiula, ameamua kuzinunulia filimbi kaya 60 kwa lengo la kujihami na matukio ya kihalifu.
dt_140616_whistle_blowing_800x600

Akiongea na gazeti la Nipashe Ijumaa hii, Mwenyekiti wa mtaa huo, alisema ameamua kuwanunulia filimbi wananchi wake ili waweze kutoa taarifa za uhalifu pindi wanapovamiwa.

“Wananchi wangu wameingiwa na hofu kubwa baada ya matukio mawili ya mashambulizi yaliyotokea…kubwa wanahofu wanaweza kuingiliwa na watu wasio wema katika nyumba zao,” alisema.

Alisema pamoja na polisi kufanya doria mara chache katika mtaa huo, lakini kama kiongozi wa wananchi hao ameamua kujitolea kuwanunulia filimbi za usalama kwa ajili ya kujitetea pale watakapovamiwa na watu wasiofahika.
Alisema filimbi ni moja ya ulinzi ambao mtu akipiga ni rahisi kufahamu kuna tukio sehemu fulani na kupata msaada wa haraka.

Alisema matukio ya uhalifu na mauaji yaliyotokea kwa kipindi kifupi ndani ya mwezi mmoja, yalichangiwa kwa kutokuwapo na ulinzi wa kuaminika, lakini kwa sasa wamejipanga kuimarisha.

Mtaa huo ulikumbwa na majanga likiwamo la mauaji msikiti wa Rahman Mei 19, mwaka huu, saa 3:00 usiku wakati wa swala ya Isha, baada ya watu waliokuwa na silaha za kijadi, mapanga na mashoka kuwavamia waumini na kuwachinja akiwamo imani wa msikiti huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents