Lady Jay Dee

Mwinyi Goha ampigia magoti Jaydee, ataka kurudi Machozi Band


Katika kile kinachoonekana kama maisha kuanza kumpiga aliyekuwa muimbaji wa Machozi Band, Mwinyi Goha baada ya kuitosa, inadaiwa kuwa amempigia magoti Lady Jay Dee na kumuomba arudi kuendelea na kazi kwenye bendi hiyo.

Mwinyi alijiondoa Machozi Band katikati ya mwaka huu kwa madai ya kuchoshwa na uongozi wa kibabe, dharau na ubabaishaji wa wamiliki wa bendi hiyo. Pia alimshutumu Jaydee kwa kuwa na roho mbaya ikiwa pamoja na kumlipa ujira mdogo ambao nao alikuwa akipewa kwa masimango.

Na sasa Kupitia Facebook, Lady Jaydee amesema muimbaji huyo ameomba msamaha na anataka arejee kuendelea na kazi.

“Nadhani wote mnamkumbuka Mwinyigoha, aliekuwa MACHOZI BAND kitambo. Baada ya yote yaliotokea na mlioyasikia anataka kurudishwa kundini, Naomba mvae kiatu changu…, Je ingekuwa wewe ni JIDE ungemsamehe na kumrudisha tena kazini?? Jiweke kwenye nafasi yangu unipe jibu,” ameandika Jide.

Kutokana na maelezo hayo bado hatma ya Mwinyi Goha kurudishwa kwenye bendi hiyo ipo mikononi mwa mashabiki wa Lady Jaydee ambao wengi wamemshauri amsamehe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents