Burudani

Mwisho Mwampamba ashtakiwa na kaka yake, kesi ipo Moro

Mwakilishi wa mara mbili wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa, Mwisho Mwampamba, anashtakiwa na kaka yake, Robert Ephraim Mwampamba kwa madai alimtukana.

page

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku 40 tangu baba yao, Dk. Ephraim Njawala Mwampamba aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) afariki dunia.

Kwa mujibu wa Global Publishers, Mwisho alipanda kizimbani kwenye mahakama ya mwanzo ya Chamwino mjini Morogoro Jumatatu hii Wawili hao wamechangia baba. Robert anamshtaki kaka yake kwa kudai alimtukana matusi ya nguoni na kumwambia maneno ya kibaguzi.

DSC_56951-1

Mwisho yupo nje kwa dhamana ya shilingi lake nne iliyotolewa na kaka yake wa tumbo moja aitwaye Isambe na kesi hiyo itasikilizwa tena April 11.

Kupitia Facebook, Mwisho ameelezea upande wa pili wa shilingi wa sakata hilo:

Kuna jamaa moja ambae cna mazoea nae hata kidogo. Si kwa salamu wala kwa shari. Amenitusi na kunikejeli kwenye group ya wanafamilia kiisha kunitafuta kupitia simu yangu binafsi ya mkononi na kuendelea kunishambulia kwa kejeli mbali mbali akitaja pia na mwanangu aisie timiza hata miaka 12. Alipopewa majibu eti yeye kaenda kushtaki polisi.ningependa jamii ifuatilie hili swala kwa ukaribu ili nijue kama kweli Tanzania tunafuata haki ama mahakama zipo kwa kukomoana. Dunia mapito tuu bila shaka kuna kitu zaidi ya hapo ila naamini kwenye ukweli kuna haki. Ila niseme mbele ya mungu kamwe sitoweza vumilia mtu atakae shambulia familia yangu itakua haina maana kuitwa mume wala baba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents