Burudani

Mzee Wenger kutunukiwa tuzo ya heshima Liberia, Wanasiasa wapingana vikali na Rais George Weah

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Arsenal, Mzee Arsene Wenger anatarajiwa kuzuru nchini Liberia Ijumaa hii ya Agosti 24, 2018 katika hafla ya kukabidhiwa tuzo ya heshima.

Image result for George weah and Wenger
Rais George Wear kushoto akiwa na Arsene Wenger enzi hizo

Rais wa Liberia, George Weah ambaye Mzee Wenger ndiye kocha wake wa zamani, atamtunuku  mzee Wenger tuzo hiyo ya heshima ambayo inatajwa kuwa na hadhi kubwa nchini humo.

Duru za habari nchini Liberia zinaeleza kuwa kumekuwa na maoni tofauti kuhusu utolewaji wa tuzo hiyo huku wengine wakisema Mzee Wenger hastahili kupewa tuzo hiyo ya heshima.

Wanasiasa nao nchini humo wanadai kuwa tuzo hiyo itatolewa kwa upendeleo kutokana na ukaribu wa toka enzi wa George Wear na Mzee Wenger.

Hata hivyo, taarifa rasmi iliyotolewa na Ikulu ya nchi hiyo imeeleza kuwa tuzo hiyo itatolewa kwa kigezo kuwa Wenger amemsaidia Wear kuonesha kipaji chake na kuitangaza vyema Liberia.

Rais Weah (51), miaka ya nyuma alishawahi kutamka wazi kuwa bila ya Mzee Wenger basi hata yeye asingeliweza kuonekana kwenye ramani ya soka barani Ulaya.

Rais Weah, ndiye mwafrika pekee kuwahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Ballon d’Or, na amekuwa chini ya kocha Wenger mwaka 1988 wakati akiwa kocha ya klabu ya Monaco na baadae wakiwa katika klabu ya Arsenal.

Related Articles

One Comment

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents