Burudani

Diamond akiniambia nimpelekee chakula popote pale alipo nitampelekea – Esha Buheti (VIDEO)

Diamond akiniambia nimpelekee chakula popote pale alipo nitampelekea - Esha Buheti (VIDEO)

Mwanadada muigizaji Esha Buheti ambaye pia ni mjasiriamali ambaye anajishughulisha na upishi wa chakula na Saloon, amefunguka mwanzo mwisho kuhusiana na kazi zake.

Mwanadada huyu amefunguka juu ya changamoto anazozipitia kwenye kazi yake ya uuzaji wa chakula na kusema kuwa “kuna kipindi unaweza kuagiziwa chakula lakini mtu asilipe au mtu anaagiza chakula yuko mbali gharama zote unatakiwa kulipa wewe kwahiyo changamoto kama hizi zinasababisha biashara kudorora”

Mbali na kufunguka hayo lakini pia ameongelea kuhusiana na ukaribu wake na Msanii alikiba pamoja na Diamond Platinumz.

Buheti alisema “Mimi namsapoti sana Alikiba lakini kwenye biashara sina utimu kwani hata familia ya Diamond Platinumz ambayo inasemwa ndio wapinzani na Ali mimi naiuzia chakula mfano mama Dangote,dada yake Diamond wote nawauzia chakula na tuna urafiki mzuri tu”

Lakini baada ya kuulizwa vipi kuhusu Diamond Alisema : “Mimi na Diamond hatujawahi kukutana na sijawahi kumuuzia chakula changu ila akihitaji chakula ntampelekea popote alipo sitaangalia U timu eti kisa mimi timu Kiba ndo nisiuze chakula hapana”

Alikiba na Diamond wamekuwa katika mchuano kwa muda sasa kwa kulinganishwa ngoma zao na jinsi wanavyofanya kazi zao na ndio maana wamejizolea mashabiki wengi sana Tanzania na hata nje ya Tanzania.

 

By Ally Juma.

Related Articles

5 Comments

  1. Aisha una tafuta kiki kwa spid sana alafu ww unelekea kwenye utu uzima sasa tazama mashavuu yalivyo anza kujikunja cku wahi kutegemea na utu uzima ume kosa buthara ivi ukiwa una gombanisha hivyo ndio uta pata nn au una dhani huyo mond ndio ata kuona wa maana ww umeamua kufanya bishara tazama nipike nn ili niongeze wateja sio kugombabisha chupi yako ina kushinda kufua una futilia mambo ya watu na uchonganishi una jiona na ww ndio dada wa mond ee acha ushamba na mm nahisi ww wa kuletwa town apa wazawa hatupo hivyo mshsmba mkubwa ww kafue chupi kwanza kisha ndio ufute ya watu ugombanishi sio dili kenge ww

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents