Habari

Nabii Owuor adai alileta Corona kuadhibu Wanadamu

Nabii ajulikanae kwa jina la David Owuor wa Kanisa la Wizara ya Toba na Utakatifu kutoka nchiniĀ  Kenya ameibuka na kutoa kauli nzito kwa Wakenya, Owuor alidai kuwa alikuwa na uwezo wa kuangamiza Nchi nzima, lakini alichagua kutafuta huruma kupitia maombi.

Owuor anasema alileta Virusi vya Corona Ulimwenguni ili kuua wanadamu wakaidi, pia amewaonya wakenya dhidi ya kubishana.

Alizungumza hayo wakati wa mahubiri katika uwanja wa Menengai mjini Nakuru, Owuor alidai kwamba Janga hilo ambalo liligharimu maisha ya watu wengi ulimwenguni, lilitokana na maneno yake ya kinabii amesisitiza kuwa wakenya waache kubishana nae juu ya uwezo wake wa kuleta maangamizi Kenya.

Kwenye hafla hiyo kulihudhuriwa na umati mkubwa wa watu, ambao uliwajumuisha watu mashuhuri wa kisiasa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents