Michezo

Mastaa Simba na Yanga kurejea

Kabla timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, kuondoka jana kuelekea Azerbaijan, kucheza mashindano mapya na mafupi ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) yajulikanayo kama FIFA Series, kilifanyika kikao kizito kati ya mabosi wa Simba na Yanga kuomba fair.
Simba na Yanga zimeliomba shirikisho hilo kuwaruhusu wachezaji wake kurejea kambini mapema ili waweze kujiandaa vyema na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tanzania’s players pose ahead of the Africa Cup of Nations (CAN) 2024 group F football match between Zambia and Tanzania at Stade Laurent Pokou in San Pedro on January 21, 2024. (Photo by SIA KAMBOU / AFP)
Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo jana alisema kuwa wamepokea maombi hayo ya Simba na tayari wameshawajibu kuwa wachezaji wale mastaa wataruhusiwa kurejea nchini baada ya mchezo wa kwanza dhidi ya Bulgaria, Machi 22.
Alisema hawawezi kuruhusiwa wote, lakini anaamini wale wenye umuhimu zaidi kwenye mechi hizo za kimataifa watarudi na wachache watabaki kwa ajili ya mchezo wa pili dhidi ya Mongolia Machi 25. Mastaa wa timu hizo waliopo katika kikosi cha Stars ni Kibu Denis, Aishi Manula, Mohammed Hussein na Kennedy Juma (wote kutoka Simba), wakati kutoka Yanga wapo Clement Mzize, Aboutwalib Mshery, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Hamad ‘Bacca’,  Mudathir Yahya.
Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents