Michezo

TFF na Al Hilal mambo yameiva

KLABU maarufu ya Al Hilal ya Sudan  itashiriki Ligi Kuu msimu ujao lakini kwa vigezo maalumu, Arena imeambiwa. Si klabu hiyo tu, hadi waamuzi wa soka wa Sudan walioko Tanzania watachezesha Ligi msimu ujao kutokana na machafuko yanayoendelea nchini kwao yaliyosababisha michezo kusimama kwa muda usiojulikana.

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), imeshakutana na kulipitisha suala hilo tayari kwa msimu ujao. Cliford Mario Ndimbo, ambaye ni Ofisa Habari wa TFF, amethibitishia kwamba Hilal itacheza kwenye Ligi Kuu msimu ujao lakini kwa vigezo maalum lengo likiwa kuongeza ushindani na kuitangaza Ligi yetu.

“Ni kweli Hilal wameomba kushiriki Ligi yetu na suala lao limeshajadiliwa na kupitishwa na Kamati ya Utendaji, kwahiyo msimu ujao watacheza mechi zote za Ligi kama timu nyingine yoyote ya Tanzania,” alisema Ndimbo. . “Tofauti yao na timu nyingine ni kwamba pointi zao hazitahesabiwa, watashiriki kama mechi za kirafiki wala kwenye msimamo hawatasomeka, TFF imewakubalia ombi lao kwavile litakuwa na faida kubwa kwenye ligi yetu.

Hilal ni timu kubwa wataitangaza ligi yetu, watatoa ushindani wa kweli kwa timu zetu, hata mapato yataongezeka kwa klabu zetu kwavile itapata nafasi ya kucheza na timu zote tofauti na awali ambapo ilicheza dhidi ya timu za Dar es Salaam tu,” aliongeza Ndimbo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents