Burudani

Nahreel aeleza kwanini hajachukua wasanii tofauti na washikaji zake wale wale kufundisha kwenye chuo chake, ‘TIMS’

Kile chuo cha muziki ambacho producer Nahreel wa The Industry amesema anakifungua ‘TIMS’, kitakuwa na walimu ambao ni washikaji zake tuliozoea kuwaona pamoja.

Nahreel

Wapo wasanii na maproducer wengi wenye ujuzi na ufahamu mkubwa wa muziki Tanzania, lakini Nahreel amewachagua wakina Nikki WA Pili, Aika, Vee Money kuwanoa wanafunzi wa ‘TIMS’ bila kuhitaji wasanii tofauti na wa familia yao.

Nahreel amesema kuwa amewachagua wao kwasababu kutakuwa na urahisi zaidi kufanya kazi wenyewe kutokana na ukaribu wao.

“Sisi wenyewe kama familia tunaweza kufanya vitu kirahisi zaidi kwasababu tumeshakuwa kama familia, kwasababu kila mtu anaelewa ile hustle mi nimetoka na Weusi mbali sana kwahiyo mi nikiwa naleta idea wenyewe watakuwa watu wa kwanza kusupport.” Alisema Nahreel kupitia 255 ya Clouds Fm.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents