HabariVideos

Naibu Waziri Katambi – Katika ustawi wa vijana, jambo la kwanza tunaangalia afya yake (Video)

Vijana wametakiwa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti 2022, ili kuhakikisha wanahusishwa kikamilifu katika mipango yote ya maendeleo inayowahusu vijana ikiwemo masuala ya Afya, Uchumi, na Siasa kwa kujua idadi yao na mikoa yao ili iwe rahisi kushughulika na ulinzi wa vijana.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi katika uzinduzi wa mpango wa kuwalinda vijana nchini Tanzania ‘Safeguard Young People Programme’ (SYP) katika sekta muhimu zinazowahusu ikiwemo suala la Maamuzi binafsi juu ya miili yao kuhusu Uzazi salama na Ushiriki wa mikakati ya kimaendeleo.

“Katika masuala yanayohusu ustawi wa Vijana, jambo la kwanza tunaangalia Afya yake, kuhakikisha Uchumi wake unaimarika na kuhakikisha Furaha yake inadumu. Na kinachofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaangalia masala haya yote yanawezekana kwa kutoa kipaombele kwao vijana na kuwajengea uwezo, kama Vijana hatupaswi kuwategemea wengine watuletee mabadiliko, bali mabadiliko yataanzia kwetu, n mabadiliko ni sisi wenyewe,” Amesema Katambi.

Aidha ameongeza kuwa Katika mipango ya maendeleo ya Miaka mitano ya Wizara yake, malengo yake ni kuhakikisha inawatambua vijana, kuwasikiliza na kuhakikisha kila hitaji lao linatimizwa na kwa mpango huu wa kuwainua vijana anatarajia vijana watahusishwa kikamilifu na baadae nchi nzima itafikiwa.

Muwakilishi wa Nchi wa UNFPA, Mark Bryan Schreiner amesema Uswisi inathamini na kuzingatia uwingi wa vijana nchini Tanzania na hivyo kurasimisha mkakati wa kimaendeleo unaohusu vijana katika nyanja ya Afya, utawala na Uchumi.

Katika salamu zake za pongezi kwa UNFPA, Muwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Zlatan Milisic amesema bila vijana hakuna maendeleo ya nchi, hakuna muungano wa pamioja katika jamii, na wala hakuna maendeleo ya nchi.

Nae Balozi wa Uswizi nchini Tanzania Didier Chassot amesema kupitia mpango huu wa pamoja kwa vijana, Ubalozi unategemea kushiriki kikamilifu kuhakikisha vijana waanapata nguvu ya pamoja katika kuhusishwa kwenye maamuzi yote ya vijana.

“Hebu fikirieni ingekuwaje ikiwa vijana wote nchini Tanzania watakuwa na afya njema, wenye tija na kuwezeshwa. Hebu fikiria wakiwa huru kutokana na magonjwa yatokanayo na ngono, pamoja na Maambukizi mapya ya VVU, mimba zisizotarajiwa na ndoa za utotoni ikiwemo aina zote za ukatili. Fikiria wakiweza kupaza sauti zao na kutetea mabadiliko. Wafikirie vijana kama viongozi wa sasa wanaoweza kuendesha uvumbuzi na ukuaji wa uchumi. Huu ndio mustakabali ambao Uswisi na nathubutu kusema UNFPA na Serikali ya Tanzania wanaufikiria.” Balozi Chassot.

Afisa Vijana wa UNFPA, Fatina Kiluvia amesema mpango huu unalenga vijana ambao ni kundi kubwa walio katika balehe kwa kuwa wao ndio wanakumbwa na madhila mengi ya kidunia.

“Vijana balehe, zaidi ya milioni 57 nchini Tanzania ndio wanatarajia kunufaika zaidi kwa sababu wao ndio waathirika wakuu wa matatizo yanayohusu vijana, wao ndio wanakumbwa na ndoa za utotoni, wao ndio wanapata mimba za utotoni, wao ndio wanaacha shule kusaidia familia kiuchumi, wao ndio wanatoroka majumbani wakiona hawaelewi mazingira yale na huko waendako wanakutana na dunia katili zaidi,” amesema Fatina.

Mpango huu wa SYP ambao utawahusu vijana kama kundi la kwanza, pia utawagusa wadau wote ambao wanahusika na vijana kama wazazi, viongozi wa dini, watunga sera, na viongozi wa mitaa na vijiji ambao ndio wakuu wa maeneo husika.
Fatina ameongeza kuwa lengo la mwishoni la mpango huu ni kuona vijana wanahusika katika utungaji wa Sera na mikakati yote ya nchi yanayohusu vijana, kuongeza uwezo na uchechemuzi wa kupanga sera rafiki kwa vijana, kuongeza ushiriki wa vijana katika kamati za maendeleo za maeneo yao, kuongeza uelewa wa elimu ya afya ya uzazi na kuongeza ujuzi kwa ajili ya maendeleo ya vijana na dunia nzima katika kupeperusha bendera ya Taifa.

“Lengo Kubwa kabisa ni kuhakikisha kijana anaweza kuruka viunzi nyote vinavyokatisha ndoto zake, kijana aelewe fursa zilizopo eneo husika na aweze kushiriki kama ni mikopo, siasa za uchaguzi, Haki za kuamua juu ya uzazi salama, na kila namna awe amelindwa,” Fatina.

Katika mjadala wa pamoja uliowahusisha vijana kutoka mashirika mbalimbali wamesema Vijana wanatakiwa kupewa ujuzi wa kufahamu kwa undani kuhusu elimu ya Afya ya uzazi, na kuhakikisha wanazungukwa na watu ambao wanaborehsa mifumo ya utawala na utoaji wa tarifa ili vijana waweze kupata urahisi wa kufanya maamuzi sahihi kutusu miili yao, waweze kupata njia za urahisi za kupata kinga na zana za kujilinda na magonjwa ya zinaa, kuzifuata na kupelekewa nafasi za uongozi, na pia kujihusisha na majadiliano yote yanayohusiana na maendeleo ya vijana.

Shirika la Kimataifa linalojihusisha na Idadi ya watu Duniani UNFPA, limezindua mpango wa kuwalinda vijana nchini Tanzania katika sekta muhimu zinazowahusu ikiwemo suala la Maamuzi binafsi juu ya miili yao kuhusu Uzazi salama na Ushiriki wa mikakati ya kimaendeleo.

Mpango huu wa kuwalinda vijana utaanza na mikoa mitano ya Tanzania Bara na visiwani ambayo ni Kigoma, Shinyanga, Simiyu, Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar na Pemba na unatarajiwa kufanyika kwa usimamizi wa Ubalozi wa Uswizi Tanzania, Serikali ya Muungano wa Tanzania na Shirika lla Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na Idadi ya watu Duniani pamoja na afya ya Uzazi, UNFPA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents