Burudani

Naumia nikiona Diamond anasemwa kila siku – Ray C

Msanii wa muziki Bongo, Ray C amesema moja ya vitu vinavyomuumiza ni kuona Diamond anasemwa kwa ‘mabaya’ kila siku.


Muimbaji huyo ametupa lawama zake katika mitandao ya kijamii kwa madai kuwa ndio inachochea hilo bila kujali Diamond amefanya mapinduzi makubwa katika Bongo Flava. Kupitia Instagram yake Ray C ameandika;

Mi naumiaga sana nikiona huyu mtoto anasemwa semwa kila siku!Amefanya mapinduzi makubwa sana huyu mtoto!kama una macho unaona!Muziki wa Tanzania umefika mbali sana sababu ya watu kama hawa!

Nigeria wanafika mbali sana kwa sababu wanasapotiana lakini Bongo sijui kwanini tunapenda kuzodoana! Kushushana! Kuchukiana! Dah!! Yani huyu alieanzisha hizi social media Mungu amlaani!!

Ray C amekuwa kimya kimuziki tangu alipotoa ngoma yake ‘Unanimaliza’ ila kwa sasa anasikika katika ngoma ‘Sema Boy’ ambayo ameshirikiana na Rachel.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents