Michezo

Nawajua Mamelodi, Yanga watashinda – Mayele

Mshambuliaji wa Pyramid FC ya Misri Fiston Kalala Mayele amewapa nafasi ya Ushindi waajiri wake wa zamani Yanga SC Kuifunga Mamelodi Sundowns na kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. “Yanga wanayo nafasi kubwa kutoboa mbele ya Mamelodi wanapaswa kujituma,
Na kucheza kwa nidhamu ili kufikia malengo waliojiwekea, Mamelodi wananikera sana wanavyocheza pasipasi nyingi, mimi nawapa Yanga nafasi kubwa ya kushinda wametoa Droo nyumbani wanaenda kuimaliza mechi ugenini, sisi Pyramid FC tulitoa nao Droo nyumbani kwao Yanga watashinda leo”.
Yanga watakuwa na kibarua kigumu leo mbele ya Mamelodi Sundowns katika Uwanja wa Loftus Versfeld huko Pretoria nchini Afrika Kusini majira ya saa 3:00 usiku, mchezo wa kwanza ulimalizika kwa droo katika Dimba la Benjamini Mkapa nchini Tanzania. Je wewe karata yako unaitupa wapi?
Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents