Burudani

Nay wa Mitego ampigia tena debe Lowassa agombee Urais 2015

Hitmaker wa ‘Nakula Ujana’ Nay wa Mitego amesema anatamani kumuona Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akigombea Urais 2015.

Nay

Akizungumza na Bongo5 leo Nay wa Mitego amesema baada ya kumuimba Lowassa katika wimbo wake Salamu Zao, amepokea maoni kutoka kwa vijana kuwa Lowassa ndiye kiongozi atakayeifaa Tanzania.

“Nikizungumzia kuhusu Lowassa yaani kila mtu anam-support,kwasababu hata ukiangalia comment za kwenye Instagram kila mtu anamadmire. Mimi sio mwanasiasa na wala siwezi siasa lakini ni mtu ambae namkubali sana .Mimi namkubali sana na kama ikiwezekana tukatuma maombi pia awepo kwenye wagombea Urais wa 2015,sijui kama yeye yupo na plan hiyo lakini vijana na mimi tumetokea kumwelewa sana na nimegundua watu wengi wapo nyuma yangu,”amesema Nay wa Mitego.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents