Habari

Ndoto Hub yawapiga msasa na kuwapatia nyenzo za biashara wanawake wajasiriamali Dar (Picha)

Jumatatu hii Ndoto Hub iliendesha program maalum yenye lengo la kuwawezesha vijana wakike kiuchumi kwa kuwapatia nyenzo za biashara za kibunifu, nafasi na maarifa ya kitaalamu yakufanyia kazi ndoto zao.

Program hiyo imehitimisha mahafali yake ya kwanza yaliyojikita kuendeleza Kilimo-Biashara na usindikaji wa vyakula ikiwa ni hatua ya kuunga mkono kwa vitendo Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004.

Ndoto Hub imefanya mahafali hayo Jumatatu wiki hii kwa kufanya ziara katika ofisi za Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ili kuweza kujifunza na kutambua fursa zilizowekwa na serikali kwa ajili ya wajasiriamali nchini.

Akizungumza baada ya Mahafali, Meneja wa programu ya Ndoto Hub, Bi. Tulinagwe Mwampanga amesema, “wamehamasika kuanzisha Programu hii kutokana nakuwepo kwa changamoto zinazowakabili wanawake wajasiriamali katika kukuza biashara zao ndani na nje ya nchi.”

Ndoto Hub inaamini katika kumuwezesha mwanamke ili kuleta maendeleo katika jamii yake na kwa chachu ya maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Aidha, katika ziara hiyo, Ndugu Edwin Chrisant, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji amewapongeza wahitimu wa mafunzo hayo na kuwahamasisha kupeleka mipango maalamu ya biashara zao ili kuweza kupata fursa ya kuwezeshwa mitaji na wadau mbalimbali.

Mahafali haya, yalihitimishwa na tafrija fupi iliyofanyika jioni katika eneo la ofisi ya
Ndoto Hub huku ikihudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo, wanawake na ujasariamli.

Katika tafrija hiyo, wahitimu waliweza kupata nafasi ya kuzielezea biashara zao kwa wageni wa waalikwa na mhitimu Aisha Uzigo, aliibuka kuwa mshindi katika maafali hiyo kwa kujishindia shilling millioni moja za kitanzaniazitakazomuwezesha kuanzisha biashara yake.

Zenna Kashaga, mmoja wa wahitimu aliwashukuru waandaji wa programu ya Ndoto Hub na kuelezea namna ilivyomwezesha kujifunza ujasirimali na kuweza kumpa mwongozo mzuri wa kujenga biashara yake, vilevile kumpa ujasiri, kujielewa zaidi na kupambanua uwezo wake yeye kama mwanamke.

Kwa sasa Ndoto Hub inawakaribisha wanawake wote wenye mawazo ya kijasiriamali katika mchepuo wa kilimo-biashara na usindikaji wa vyakula kutuma maombi ya kujiunga kupitia www.ndotohub.com.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents