Burudani

New Music & Lyrics: Mkoloni – Tupo Pamoja

Ngoma mpya ya Mkoloni inaitwa ‘Tupo Pamoja’ iliyotayarishwa na Jors Bless na Hermy B.

Utangulizi:

Wanafunzi habari zenu? Someni vizuri nyie Taifa linawategemea.
Vijana,nyie ndio nguvu kazi ya Taifa
Wazee wangu heshima zenu,
Wakina mama jamani jamani dooh!
Madereva wa bodaboda Mimi ndio mtetezi wenu ,eeh nitawatetea,eeh kabisa!

Ubeti wa kwanza:

Hii sauti kila mtu ambaye ataisikia,
Moja kwa moja kashajua ni kitu gani kinafwatia,leo ni elimu ya bure nimeamua kuwapatia,nia yangu watanzania tusije kupotea njia,haya maisha kila jambo halikosi sababu,kila mmoja wenu ana maswali na hayana jawabu,mtambue viongozi wamekalia kuti kavu,mwezi wa oktoba ni lazima tuwashikishe adabu,tumeshakula ng’ombe mzima tumebakisha mkia,hizo ajira tu hatujui hata zinavyonukia,ahadi ngapi zimetolewa na ngapi zimetimia? Mambo mengine wananchi sie wenyewe tunajitakia,sawa ni ngumu kubadili upepo hasa unapovuma,lakini Mungu katupa akili tunatakiwa kujituma,turekebishe tanga chombo kiende tunapotaka,sio kujitosa baharini tu tena haraka haraka.

Kiitikio:

“DJ D ommy’s scratch…ja..ja..ja…..
“Jamani hamjambooooo…tu..tu…tu…
“Tupo pamoja…..ni…ni..ni……
“Nikilima na wapiga kura….po..po…po..
“Potelea mbali”…………

Ubeti wa pili:

Enheeee nimekumbuka kabla hata sijasahu,sasa hivi wagombea meno nje hawaonyeshi dharau,si wanataka cha uvunguni ni lazima wainame,jamani hamjambooo? Tupo pamojaaa,nawaambieni mwaka huu tutashuhudia vihoja,hata shambani atakajua na mtalima pamoja,baada ya hapo ni picha zinazagaa mitandaoni,”nikilima na wapiga kura” hatupo ndotoni,miaka yote hiyo haujaonekana jimboni,ndio unakuja na siasa zako kutulaghai mwishoni,tufanye maamuzi sahihi sio kama mwanzoni,majuto ni mjukuu hii kauli ikumbukeni,yaani uongozi siku hizi umekuwa kama ni mtaji,pisheni wenye nia safi nafasi wanazihitaji,waheshimiwa hilo bunge linaitwa bongo movie,nimeikopi na kupesti wala sijaongeza chumvi.

Rudia kiitikio: (kama cha mwanzo)

Ubeti wa tatu:

Watanzania oyeeee!!! (Oyeeeee!!)
Mtanichagua??? (Ndiyooo!!)
Iwe ndiyo ya ukweli sio ya kofia na flana,au vishilingi elfu mbili mbili na pilau ya nyama,wengine wanafwata mkumbo hakuna wanachokijua,wapo wanaosema siasa za bongo zinazingua,baadhi ya watu ndio kabisa hawana hata habari,wao akishinda yeyote utawasikia “potelea mbali” ,kwa taarifa yako kura yako inabadili maisha yako na kiongozi wako ndio anakuwa chanzo cha maendeleo yako,haya masuala ni mazito yanahitaji busara,juwa chama,sera na ilani msifanye papara,tutaona mikutano na kushuhudia maandamano,kikubwa tuombe Mungu yasitokee mapigano,japo kila tunavyokwenda tunakiuka maagano,mpiga kura ndio refa sasa tuanze pambano!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents