Habari

Ni kweli Tanzania ilikuwa ni zaidi ya ‘shamba la bibi’?

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani zilizobarikiwa kuwa na rasilimali nyingi.

2016-01-10-1452455825-8283801-JohnMagufuli

Japo Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo nchi nyingine hakuna kama; madini ya Tanzanite, vyura wa Kihanzi, n.k. Lakini rasilimali zilizopo kwenye nchi hii na maisha ya wananchi ni vitu ambavyo havilingani kabisa.

Viongozi wengi wasiokuwa waaminifu wameshindwa kuwajibika ipasavyo kwenye kazi zao, wamejirundikia mali na kusahau wito wa kuwatumikia wananchi. Hakika kauli ya ‘Hapa Kazi Tu’ imewaamsha viongozi wazembe waliolala na kujisahau.

Kwanini uweze kumiliki nyumba zaidi ya thelathini peke yako kwa kuiba mali za umma wakati wananchi unaowatumikia wana kufa kwa kukosa dawa wakienda hospitali, yule mwanafunzi wa Chunya anaenda shule bila viatu na anakaa chini kwa kukosa dawati?

Lady Jaydee aliimba, “Machoni kama watu, moyoni hawana utu,” wanapokuja kwa wananchi wanakuwa na ngozi ya mbuzi lakini wanapoondoka wanaivua na kubaki na ngozi yao ya chui.

Agizo la Rais Magufuli kwa wakuu wapya wa mikoa kwa kuandika majina ya wafanyakazi hewa ambao wapo kwenye mikoa yao, hutaweza kuamini wala kusikia kilichopo. Haiwezekani nchi kama Tanzania inaomba misaada nje kwa ajili ya bajeti ya serikali wakati inatumia bilioni tatu kila mwezi kuwalipa mishahara wafanyakazi hewa ambao ni zaidi ya 3000.

Tumeona mikataba mingi ambayo serikali imeingia haiwanufaishi wananchi. Hata wabunge waliotegemewa na wananchi na kuchaguliwa wakiwa hawana hata miezi sita mpaka sasa wanatuhumiwa kwa sakata la rushwa. Kama wameshindwa kwa kidogo je wakipewa kikwabwa watafanyaje?

“Kule Dar es Salaam kwenye ofisi ya TRA kuna mfanyakazi mmoja analipwa mishahara ya wafanyakazi hewa 17,” alisema Rais Magufuli alipokuwa Chato kwenye mapumziko yake.

Unakumbuka yale makontena zaidi ya 300 yalivyopitishwa bandarini bila kulipiwa kodi? ‘Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni’, kwanini nchi ya India iwe ndiyo nchi ya kwanza kwa kuuza madini ya Tanzanite wakati yanapatikana kwenye ardhi ya Tanzania pekee?

Rais Magufuli anajitahidi kurudisha uwajibikaji kwa viongozi serikalini, lakini tukumbuke kuwa ‘kidole kimmoja hakivunji chawa’, kila mtu anapaswa kuwa na utayari wa kuwajibika kwa hili. Hatuhitaji kuendelea kuomba misaada nchi za nje kwa kupewa masharti magumu yanayonya rasilimali zetu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents