Burudani

Nikki Mbishi, One na Songa kupiga tour ya muziki pamoja

Licha ya kutangaza kuachana na muziki, Nikki Mbishi amesema anakuja na tour ya muziki atakayokuwa pamoja na Songa na One The Incredible.

1507900_828526730502777_4706909768576165335_n

Nikki ameiambia Bongo5 kuwa ziara hiyo haitotegemea matangazo makubwa ila wao wenyewe watatumia nguvu zao ili kuwafikia mashabiki wa muziki wao.

“Binafsi kipo kitu nimekipanga ambacho ni tour ambayo itakuja nitakuwa na Songa, Stereo, nitakuwa na One pengine ndo muda pekee ambao mimi nitakutana nao tena na kuzungumza nao yale yaliyonisibu katika ile hali ambayo tunaitengeneza kutaka kupeleka muziki kule tunapotaka uende,” amesema Nikki.

“Itakuwa sio busara kuwapachikia mangoma kibao ya zamani na sisi sidhani tena tunahitaji radio kwaajili ya kusikika. Sisi hatuna muda huo. Sasa hivi tunafanya jitihada za kufikisha nyimbo zetu kwa watu bila kuingiliwa na mtu, sio mpaka radio au TV au uende wapi. Watu wanaweza wakaweka ngoma mtandaoni tu na zikawafikia watu wetu. Kutoa ngoma muziki ni maisha yangu mimi. Mimi ninaweza nikauchukua muziki wangu niliourekodi 2005 wewe haujui, nikaamua kuuweka Mkito, wakasema Nikki Mbishi katoa wimbo mpya lakini sio ngoma mpya. Mimi naachia mangoma kibao ambayo yapo niliyarekodi zamani, sisemi kwamba nitatangaza kwamba watu wawe attention Nikki anarudi no,” ameongeza rapper huyo.

Kwa upande mwingine, Nikki Mbishi amesema baada ya kutangaza kuachana na muziki, ametambua ana umuhimu gani katika muziki wa Hip Hop Tanzania.

“Kwa haraka haraka hii ni namna ya kutafuta takwimu watu wangapi wapo pamoja na wewe kwahiyo mara nyingine ili upate kusikika na watu kwa kile unachokifanya ni lazima utafute usikivu kwanza. utayari wa watu hao kukusikiliza. Kwahiyo mimi nilijaribu kuangalia OK nafanya hii kazi najifurahisha? Je hawa watu wanakithamini ninachokifanya? Kwahiyo hiyo kwa namna moja ama nyingine inaweza ikani-motivate mimi ikanipa mimi ari nyingine ya kusema hapana kumbe bado uwezo ninao, kwa sababu watu wamekubali kile ninachokifanya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents