Burudani

Nikki wa Pili ashtushwa na mabadiliko ya gharama za ada zitakazotozwa na BASATA ‘kifupi dili zitakufa’

Rapa Nikki wa Pili ameshangazwa na tozo za ada ambazo yanachajiwa Makampuni pale yanapotaka kufanya kazi na  wasanii wa muziki nchini Tanzania.

Nikki wa Pili

Nikki wa Pili kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa tozo watakayolipa Makampuni itakuwa ni kilio kwa wasanii kwani hakuna kampuni itakayokubali kulipa shilingi milioni 5 kwa kufanya kazi  na wasanii.

Matangazo yapo ya aina nyingi, kampuni inaweza mtumia msanii kuposti tangazo lao katika page yake, waka mlipa kwa post moja au mbili, sasa ukisema hapo kampuni ilipe basata milioni 5?? sasa kwani kwa post moja msanii hulipwa bei gani, kifupi hapo hizo dili zitakufa,“ameandika Nikki wa Pili.

Mnamo Julai 04, 2018 Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Lilitangaza kuwa Makampuni yatakayotumia wasanii au sanaa kujitangaza (Branding) yatatozwa gharama ya shilingi laki 5 huku matangazo yatakayotumia wasanii kila tangazo/tukio litatozwa shilingi milioni 5.

SOMA ZAIDI – BASATA watangaza mabadiliko ya bei za usajili, MaDJ na Wasanii wapumua, Makampuni bei juu

Related Articles

Back to top button