Nimerudi nyumbani, klabu iliyonilea (+Video)

Msemaji wa Yanga SC, Haji Manara amewashukuru wazee wa timu hiyo waliyompkea na kusema kuwa amerudi nyumbani, klabu ambayo imemlea.

Manara ameyasema hayo alipofika Makao Makuu ya Yanga kwa mara ya kwanza baada ykujiunga nao na kukabidhiwa ofisi.

“Nimerudi nyumbani sehemu ambayo imenikuza, mnafahamu wazazi wangu licha ya kucheza hapa lakini bado ni Wanachama wa Klabu hii na mimi kurudi hapa ni fahari kwamba narudi kufanya kazi katika klabu ambayo ilinilea na ndiyo Klabu ya maisha yanga. Ndugu zangu katika siku ngumu ni ambayo unapokewa na watu ambao wewe unastahili kuwapokea, kwa mila na desturi zetu Afrika wazee wanapokewa na vijana, lakini kwa umaalum mlionifanyia leo ni deni zito, sijawai kupata mapokezi mazito kutoka kwa wazee wangu kama siku ya leo, deni hili pia ninalo kwa Wanachama wote wa Yanga nchi nzima” Msemaji wa Klabu ya Yanga

Related Articles

Back to top button