Habari

Nimeshtushwa na tukio la bomu kwenye Ofisi ya Mawakili – Zitto

Baada ya Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya kuthibitisha kushambuliwa ofisi za wanasheria za IMMMA saa 8 usiku wa kuamkia leo, Agosti 26.

Hatimae Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameshtushwa na tukio hilo lililotokea katika ofisi ya Mawakili wa IMMMA advocates.

Nimeshtushwa na tukio la bomu kwenye ofisi ya Mawakili wa IMMMA Advocates. Wakati tunaendelea kupata Taarifa zaidi nawasihi wanasheria wa kampuni hiyo kuwa na moyo wa subra na ninawapa pole Sana.
Kuna haja ya uchunguzi Huru kuhusu matukio ya aina Hii kwani yanamwelekeo fulani. Tukio kama hili lilitokea Kwa Wakili Omar Said Shaaban ambaye alikuwa anamtetea Ndugu Mansour Yusuf Himid. Sasa aina hiyo hiyo ya uhalifu imefanywa dhidi ya ofisi anayofanya kazi Wakili Fatma Karume ambaye ni mpwa wa Mansour. Tusiache mambo haya kuzoeleka hata kidogo.

Hata hivyo Kaimu Kamanda, Lucas Mkondya amesema kuwa wapo hapa eneo la tukio, uchunguzi unaendelea na ukikamilika tutawapa taarifa zaidi.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents