Burudani
Nipo tayari kuchanwa na msanii yeyote – Young Killer
Wasanii hutumia mashairi yao kufikisha ujumbe kwa jamii lakini wengine hutumia hiyo hiyo mistari kumchana mwenzake kama wanavyofanya Drake na Meek Mill kwenye nyimbo zao.
Akiongea kwenye kipindi cha E News, kinachoruka kupitia EATV, rapper huyo kutoka Mwanza, alisema yupo tayari kuchanwa na msanii yeyote.
“Kama mtu anataka kunichana kwenye wimbo wake anichane tu mimi nipo tayari ila kumbuka kuwa na mimi nachana pia tena nachana sana,” aliongeza.
Wiki hii Young Killer ameachia wimbo wake mpya ‘Kumekucha’ aliomshirikisha Mr Blue.