Burudani

Nisingekuwa msanii ningekuwa mwanajeshi – Barakah The Prince

Msanii wa muziki Bongo, Baraka The Prince amedai iwapo asingeingia katika fani hiyo basi angekuwa mwanajeshi.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Sometimes’ amekiambia kipindi cha Eight cha TVE  kuna vitu visivyopungua vitano ambavyo vinamvutia kutoka kwa wanajeshi.

“Napenda mazoezi, napenda ule mchaka mchaka, napenda yale mavazi yao, napenda ile attitude yao, napenda ukarimu wao, yaani napenda the way walivyo,” ameema Baraka The Prince.

Barakah The Prince kwa sasa anafanya kazi zake chini ya label yake mpya Bana Music baada ya kuondoka RockStar4000 mwishoni mwa mwaka jana. Mwaka 2015 alishinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards (KTMA) kama msanii bora anayechipukia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents