HabariVideos

NMB yafungua dirisha la kupokea maombi ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi Sekondari mpaka vyuoni (+ Video)

Siku ya leo benki ya NMB imefungua rasmi dirisha la kupokea maombi ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu kupitia ‘Nuru Yangu Scholarship and Mentorship Program’.
Akiongea na wana habari Mwenyekiti wa Bodi ya NMB Foundation – Ruth Zaipuna amesema ufadhili huu unawalenga wanafunzi waliofanya vizuri na wanaotoka kwenye familia zenye changamoto ambao watapata ufadhili wa kusomeshwa bure kwa mwaka 2022/2023 – ikiwemo kulipiwa gharama za ada, vitendea kazi na nauli.
Jumla ya wanafunzi 200 watanufaika na programu hii, ambapo 50 watakua wa masomo ya shahada (undergraduate) na 150 wa kidato cha tano na sita (A-level).
Programu hii inatekelezwa chini ya NMB Foundation.
https://www.youtube.com/watch?v=0yeRdPvbk9c

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents