Burudani

Nyimbo zangu nyingi ni classic sababu hazikupata video mbaya – Jay Moe

Rapper mkongwe, Jay Moe amesema sababu inayozifanya nyimbo zake nyingi kuwa classic ni kuwa hazikuwahi kuwa na video na hivyo kuepuka kuwa na video mbovu kutokana na kutoka katika kipindi ambacho hakukuwa na production nzuri za video za muziki.

13642901_313507408995872_34383676_n

Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, Moe alidai kuwa huenda angelazimisha kufanya video za ngoma kama ‘Kama Unataka Demu’, Bishoo, Mvua na Jua, Famous na zingine, angepata mbovu ambazo zingeharibu ukubwa wa ngoma hizo.

“Nilikuwa najikuta naweza nikakaa chini na director fulani tujadili kuhusu hiyo music video lakini baadaye namna moja au nyingine nikajikuta labda haitakuwa vile kama ambavyo mimi nilidream itakavyokuwa,” alisema rapper huyo.

Ametolea mfano wimbo wake Famous ambao alikuwa na nia ya kuifanyia video lakini aliahirisha baada ya kuona mazingira yasingemruhusu kupata kitu bora kinachostahili ukubwa wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents