Burudani
Omarion na girlfriend wake wanatarajia kupata mtoto wa pili
Mwimbaji wa R&B wa Marekani ambaye ni baba wa mtoto mmoja, Omarion na girlfriend wake wa muda mrefu aitwaye Apryl Jones wanajiandaa kumpokea mtoto wao wa pili.
Mwimbaji huyo wa ‘Post to Be’ ametumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kushare na mashabiki wake kuwa girlfriend wake ni mjamzito na anatarajia kujifungua mtoto wa kike.
“My lil princess is on the way. #5monthspreggoanduainteeknooit,” alitweet Omarion.
Mtoto wao wa kwanza ambaye ni wa kiume waliyempa jina la Megaa Omari Grandberry alizaliwa August 2014.