Burudani

Ommy Dimpoz akanusha taarifa ya gazeti la Ijumaa kuwa alimkashifu Ngwair, GP nao waongea (audio)

Hitmaker wa Me and You Ommy Dimpoz amefunguka exclusively kwa Bongo5 kuhusiana na habari iliyoandikwa kwenye gazeti la udaku la kila ijumaa kuwa amemtukana Mangwair.

BMtID8cCMAEQKwK

“Kifo cha Ngwair, kilivuta makundi mbalimbali kushiriki kwa hali na mali kuchangia na kumzika, taifa lilizizima mkoa kwa mkoa, mguso huo wa kitaifa aliokuwa nao mwanamuziki huyo, Ommy hakuuona, isipokuwa akanena: ‘Sitaki kufa maskini kama Ngwair’ limeandika gazeti hilo.

Ommy amekanusha kusema kauli hiyo na kudai kuwa habari hiyo imeandikwa baada ya kushindwa kuelewana malipo ya show waliyomtaka akatumbuize.

“Watu wa Global Publisher wana tamasha lao la Matumaini, kwahiyo wakanipigia simu wakataka nifanye nao show kwahiyo tukawa tunabargain kuhusu bei. Wakati tunabargain kuhusu bei nikawa nimewaambia kwamba mimi nahitaji kiasi fulani, tukabishana bishana, mwisho wa siku hatukuafikiana. Baada ya pale wakakata simu, matokeo yake limekuja kutoka hilo gazeti,” amesema Ommy.

Ameongeza kuwa gazeti hilo limetumia kauli aliyoisema siku ya KTMA 2013 aliposema kuwa amechoka kuona wasanii wanakufa maskini wakati kuna makampuni mengi yanayoweza kuwapa mikataba na kufanya nao kazi ili wawe na maisha mazuri.

“Kwa mtu anayenifahamu kama Ommy na watu ambao wamefanya kazi na mimi wananielewa vizuri lakini ukiangalia habari yao nzima imekaa katika misingi ya kiuchochezi. Wao wameamua kinichafua sababu tulikuwa tupo kwenye mazungumzo ya kibiashara na hatukuafikiana.”

Ameongeza kuwa wakati wamempigia simu mara ya pili walikuwa wakimuuliza maswali ili kutengeneza majibu ya kumchafua baadaye.

“Kwanza mimi ni muislamu, najua hata maiti akishakufa jinsi ya kumuongelea kwahiyo wao walikuwa wananitengenezeshea kauli. Nikasema hapana, mimi nilichozungumza ni kwamba kama kweli tunataka tuendelee na hii sanaa basi ninyi pia muwe mifano mizuri ya kutulipa vizuri kwasababu tunatumia nguvu nyingi kuinvest.”

Kwa upande wa Mkurugenzi mkuu wa Global Publisher, Abdallah Mrisho amekanusha kuwa gazeti la Ijumaa halijaandika habari hiyo kwa nia ya kumchafua ama kumkomoa Ommy baada ya kushindwa kuafikiana bei ya kumlipa kwenye tamasha la Matumaini. Mrisho amesema tamasha la Matumaini linaandaliwa na menejimenti tofauti ambayo haihusiani na masuala ya editorial.

“Labda issue ingekuwa story iliyoandikwa si ya kweli labda issue ndio ingekuwa hapo,” Mrisho ameiambia Bongo5.

Waskilize wote hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents