Burudani

Orodha kamili ya vijana wenye ushawishi Africa, Nancy Sumari na Jokate ndani

Baada ya utaratibu wa kutaja jina moja moja hapo jana, hatimaye mtandao wa African Youth Awards umetoka orodha kamili ya majina 100 ya vijana walio chini ya umri wa miaka 40 wenye ushawishi zaidi barani Afrika kwa mwaka 2017.

Nancy Sumari na Jokate

Awali jana mastaa wa muziki kutoka Tanzania, Alikiba na Diamond Platnumz walitajwa kwenye orodha hiyo pamoja na muigizaji wa filamu nchini Tanzania mrembo Elizabeth ‘Lulu’ Michael na mwanamitindo Flaviana Matata.

Usiku wa kuamkia leo mtandao huo umetoa urodha kamili huku Miss Tanzania 2005 ambaye pia ni Miss Dunia wa Afrika 2005, Nancy Abraham Sumari akitajwa pia kwenye orodha.

Pia mjasiriamali na mwanamitindo Jokate Mwegelo ametajwa pia kwenye list hiyo.

Kwa upande mwingine wasanii waliochaguliwa kwenye orodha hiyo kutoka nje ya Tanzania ni Davido kutoka Nigeria , Rapa AKA kutoka Afrika Kusini na wengine wengi.

Dirisha la kupendekeza majina ya vijana wenye ushawishi zaidi barani Afrika mwaka 2017 lilifunguliwa mwezi June 25 na kufungwa agosti 22 mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents