Habari

Oscar Pistorius apelekwa mahakamani kukabiliana na kesi ya mauaji ya mpenzi wake

Oscar Pistorius covering face at police station

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius leo amepelekwa mahakamani kusomewa mashtaka ya mauaji ya mpenzi wake.

Waendesha mashtaka wamesema staa huyo anakabiliwa na kesi ya kuua kwa kukusudia “premeditated murder”.Mpenzi wake mwanamitindo Reeva Steenkamp alipigwa na risasi na kufa nyumbani kwa Oscar jijini Pretoria jana.

Mrembo Reeva aliyeuliwa na mpenzi wake Oscar
Mrembo Reeva aliyeuliwa na mpenzi wake Oscar

Pistorius alionekana kuinama chini muda mwingi huku akilia wakati kesi yake ilipokuwa ikisomwa.Maombi ya dhamana yameahirishwa hadi Jumanne ijayo ambapo Pistorius, 26, ataendelea kubaki kwenye kituo cha polisi badala ya kupelekwa gerezani.

Hakimu katika kesi hiyo amesema vyombo vya habari havitaruhusiwa kurusha live kesi yake.Dada yake Aimee, kaka yake Carl na baba yake Henke, nao walikuwa mahakamani hapo.

Oscar anadaiwa kumuua mpenzi wake akidhania kuwa ni jambazi.Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zenye matukio mengi ya kihalifu duniani na wananchi wengi wanamiliki silaha ili kujilinda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents