Habari

OSHA yatoa msaada wa vifaa kinga kwa watu wenye ulemavu (+Video)

Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umetoa msaada wa vifaa kinga kwa wanachama wa Chama cha Wasioona Tanzania ili kuwawezesha kujikinga na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID 19) unaosababishwa na virusi vya Corona.

Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwa viongozi wa chama cha Wasiona Tanzania hicho ni pamoja na vitakasa mikono (sanitizers), barakoa, ndoo za kuniwia mikono kwa maji tiririka pamoja na sabuni za maji.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa viongozi wa chama, Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema OSHA kama taasisi ya serikali yenye jukumu la kuhakikisha maeneo ya kazi yanakuwa salama, wameguswa na changamoto kubwa inayolikabili kundi hilo maalum katika kujikinga na ungonjwa wa Corona.

Aidha, aliwaomba wadau wengine kujitokeza na kutoa misaada zaidi kwa makundi ya watu wenye ulemavu ili nao waweze kujikinga na kuendelea kushiriki katika shughuli mbali mbali za ujenzi wa Taifa.

Wakitoa shukrani zao mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo muhimu, viongozi wa Chama cha Wasioona Tanzania, Bw. Omari Itamba na Paul Zumba wameishukuru OSHA kwa masaada huo muhimu kwa wanachama wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents