Burudani

P-Square waanza kurekodi kazi mpya

Baada ya miezi kadhaa ya kutoelewana na kusababisha kuvunjika kwa kundi la P-Square sasa, Peter na Paul Okoye wameanza kurekodi kazi mpya.

12940912_1799083410377084_825748254_n

Mwezi Julai mwaka huu member wa kundi hilo Peter Okoye aliandika ujumbe kwenye Instagram akiwaomba msamaha mashabiki wao kwa kuvunjika kwa kundi hilo lakini aliwaahidi kuwa P-Square linarudi tena na alitangaza kumrejesha kaka yao, Jude Okoye kama meneja wao.

Kupitia akaunti ya Instagram, Peter ameandika ujumbe unaoonyesha kuwa kuna kitu kipya anarekodi studio na ndugu yake Paul.

Something new Cooking in da kitchen and about to come out! From us! You already know it’s P2 baby!!! #KoolestDudes

Kurudi upya kwa kundi hilo ni ndoto ya kila shabiki wa muziki Afrika kutokana na heshima kubwa waliojitengenezea kipindi walipokuwa pamoja. Muda ndio utaongea tusubiri tuone.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents