HabariMichezo

Pacome aishukuru Yanga

Kiungo wa Yanga Pacome Zouzoua amefanikiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Taifa lake Ivory Coast kwa mara ya kwanza.

Pacome amejumuishwa kwenye kikosi hicho kinachojulikana kama Tembo kinachoenda kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika yatakayofanyika nchini Ivory Coast, ingawa amewahi kuizitumikia timu za Taifa kwa vijana lakini haikuwa rahisi kuitwa timu ya wakubwa.

“Msimu uliopita nilikuwa mchezaji bora wa Ligi ya Ivory Coast lakini sikupata bahati kama hii, ndani ya muda mfupi nikiwa hapa Yanga naitwa timu ya Taifa hii ni bahati nawashukuru sana Yanga” aliongea Pacome Zouzoua.

Je, ni sahihi kuwa Ligi Kuu ya Tanzania ina ushawishi zaidi na kuvutia wachezaji wa kigeni kadri siku zinavyoenda?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents