Habari

Padri aliyewanyanyasa watoto kingono afia gerezani (+ Video)

Padri wa zamani wa Kanisa Katoliki ambaye alifungwa jela kwa kuwanyanyasa kingono watoto watatu pamoja na mwanafunzi aliyekuwa akisomea upadri amefariki jela.

Paul Moore, ambaye alikuwa na umri wa miaka zaidi ya 75, alitekeleza uhalifu huo katika maeneo tofauti mjini Ayrshire kati ya mwaka 1977 na 1996.

Alifungwa miaka tisa jela kufuatia uchunguzi wa BBC, lakini kifungo hicho kilipunguzwa hadi miaka minane na majaji wa mahakama ya rufaa.

Uhalifu wa Moore ulichukua zaidi ya miaka 20 kujulikana na mmoja wa wahasiriwa alikuwa na miaka mitano.

Msemaji wa Dayosisi ya Galloway alisema: “Askofu Nolan ataombea roho ya Paul Moore msamaha na amani kwa wale walioteseka katakana na kitendo chake.

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CL6TJqMhzfR/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents