Habari

Picha: CUF yawakumbuka wanachama wake waliouawa mwaka 2000 Zanzibar

Chama cha wananchi (CUF) Ijumaa hii kimeadhimisha kumbukumbu ya miaka 17 ya wahanga walioteswa na kuuawa January 27, mwaka 2000 huko visiwani Zanzibar.


Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba akizungumza kwenye maadhimisho hayo katika makao makuu ya Chama hicho yaliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mgombea nafasi ya makamu mwenyekiti CUF taifa, Mussa Haji Kombo


Mohamed Abibu Mnyaa aliyekuwa mbunge wa Mkanyageni Pemba akizungumza

Sababu ya kutokea mauaji hayo ni kutokana na chama hicho kutaka uchaguzi wa mwaka 2000 urudiwe. Tume ya uchaguzi ilikataa na kutaka yarudiwe majimbo 16 tu na si uchaguzi wote japo ambalo CUF ililipinga.


Naibu mkurugenzi wa mipango na uchaguzi, Jaffary Mneke akizungumza na wananchi


Wananchi wakisikiliza kwa makini kilichokuwa kinaendelea

Profesa Lipumba alisisitiza kuwa walifanya maandamano hayo kwa amani.


Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho hayo


Mwanachama halisi wa CUF ambaye alivaa t-shirt yenye ujumbe mzito, akionesha kuwa na mapenzi ya dhati na chama hicho

Watu zaidi ya 60 walipoteza maisha na wengine 2000 walikimbilia Shimoni mjini Mombasa kufuatia vurugu hizo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents