Burudani

Picha: Mapenzi ya Chris Brown na Karrueche Tran yarudi kwa kishindo, ni baada ya kudaiwa kuachana

Bila shaka nuru ya mapenzi imerejea katika mioyo ya mwimbaji Chris Brown na model Karrueche Tran, baada Breezy kuthibitisha kuwa button ya uhusiano wao imerudi ‘on’.

breezy1

Couple hiyo ya ‘On & Off’ imeonekana ikiwa na furaha baada ya Breezy kupost picha wakiwa pamoja kwenye mechi ya mpira huko L. A Jumapili (Agosti 17). Pamoja na kwamba Chris hakuweka caption yoyote lakini nyuso zao tu zinathibitisha kuwa wamerudiana.

breezy2

Hivi karibuni Karrueche alidaiwa kumuacha Chris Brown, na miongoni mwa sababu zilizotajwa ni pamoja na kuwa Karrueche amekuwa hana furaha kutokana na Chris kufanya mambo yake kama mtoto, na pia kutumia muda wake mwingi kula bata badala ya kutengeneza muziki.

Vyanzo vingine vilidai kuwa Breezy ndiye aliyemuacha Tran na miongoni mwa sababu zilizotajwa ni kuwa amekasirishwa kwa kitendo cha Tran kuzungumzia uhusiano wao kwenye Interviews pamoja na Clothing Line yake, kwa lugha nyingine anaona kama anatumia mambo yao kupata attention imsaidie kibiashara (opportunist).

Chris Brown cuddles up to on/off girlfriend Karrueche Tran as they attend his charity footbal game in Los Angeles, CA

breezy3

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents