Habari

Picha: Spika Ndugai alivyokutana na Watendaji wakuu wa BOT

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amekutana na kuzungumza na Watendaji Wakuu kutoka BOT na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika.


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma

Tazama picha zaidi:

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akimsikiliza Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma wakiongozwa na Gavana wa Benki hiyo, Prof. Florens Luoga (kushoto kwa Spika). Kulia kwa Spika ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (kushoto) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga (kulia) baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (watatu kushoto chini) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) walioongozwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga (watatu kulia) baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kushoto chini ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Mhe. Stephen Masele (kulia) ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Mbunge wa Shinyanga Mjini, Mhe. Stephen Masele (kulia) ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma

PICHA NA OFISI YA BUNGE

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents