Burudani

Profesa Jay aeleza kuumizwa kwake na kuendelea kwa wizi wa kazi za wasanii

Msanii maarufu wa Hip Hop nchini , Profesa Jay ametoa kauli ya kuonesha kuumizwa na wizi wa kazi za wasanii huku akidai kama mamlaka husika zimeshindwa kutatua tatizo hilo.

1378217_10151896306867558_1516010385_n

Kupitia Facebook Profesa ameandika:

Tatizo kubwa na la miaka nenda rudi kwenye SANAA Yetu iwe Muziki,Filamu na sanaa nyingine ni WIZI wa waziwazi wa kazi zetu, Inauma sana unapopita Ubungo Mataa, Mwenge, na sehemu mbali mbali za katikati ya jiji na kukuta ndugu zetu kabisa wakiuza kazi mpya za wasanii mbalimbali ambazo sio ORIGINAL na bila ridhaa ya wasanii wenyewe.Mbaya zaidi ni pale tunapowakamata na kuwapeleka polisi kesho yake unawakuta wameachiwa na wanaendelea na kazi yao na ukiwahoji ni nani anayetengeneza hizo CD na DVD hawataji kamwe.

Pia kuna wale ambao wana vibanda vyao vingi nao pia utakuta bila aibu wameweka matangazo..Tunaburn nyimbo mpya za Bongo Flavour, Bongo Movies.. CD,DVD,Tunaingiza nyimbo kwa Bluetooth na kwenye flash kwa bei Karibu na bure, Mbaya zaidi imekuwa kama ni halali kwao wakati hilo ni jasho la msanii na kimsingi hanufaiki nalo hata kidogo.

Je kweli tumeshindwa kulitatua hili TATIZO SUGU Au mpaka wasanii tuchukue SHERIA mikononi kama madereva wa BODA BODA ndio mtakisikia hiki kilimo chetu?? Bado siamini kama tunatakiwa kufika huko.. Nawaomba sana ushauri wenu nini kifanyike??? Mungu ibariki sanaa yetu Mungu ibariki TANZANIA!!! ASANTENI. Kutoka kwa PROFESSOR JAY To the WORLD.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents