HabariSiasa

Raila Odinga apiga kura katika kituo cha Old Kibera

Mgombea urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga alifika katika kituo cha Old Kibera kutekeleza haki ya yake ya kidemokrasia.

Raila ambaye alikuwa akielekea katika kituo cha kupigia kura, msafara wake ulikutana na umati wa wafuasi wakimsubiri.

Raila Odinga akishangiliwa na watu wakati anakwenda kupiga kura

Raila alifika katika kituo cha kupigia kura baada ya nne asubuhi.

Alikuwa ameandamana na mkewe Mama Ida Odinga.

Wakati anatoka kwenda kupiga kura, Raila alizungumza na vyombo vya Habari na kusema kwamba ‘’wamefanya kadiri ya uwezo wao na sasa kibarua kilichobakia ni kwa raia’’.

Pia ameiriki kusikia baadhi ya changamoto zinazokumba maeneo ya kupiga kura.

Mkewe Raila Odinga Bi. Ida Odinga naye alikiri kwamba ni zoezi analolifurahia kama Wakenya wengine kwa sababu hutokea mara moja kila baada ya miaka.

Related Articles

Back to top button