Habari

Rais Magufuli ameagiza JKT kurejesha ardhi kwa wanakijiji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kurejesha eneo la eka 50 walilopewa na Kijiji cha Mkata, baada ya kushindwa kuliendeleza kwa miaka 7.

Rais ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na wananchi wa Mkata akiwa njiani kuelekea mkoani Tanga, ambapo alimwita Mkuu wa JKT wa eneo hilo na kumhoji kuhusu kuendeleza eneo hilo.

“Hili eneo tangu mmepewa ni miaka mingapi sasa? Mliomba ili mjenge muwekeze kwa kujenga kiwanda, lakini mmeshindwa sasa leo hii mrejeshe kwa wananchi ili waweze kumpa hata mwekezaji mwingine,” ameagiza Rais Magufuli na kushangiliwa na wananchi.

Hata hivyo Rais Magufuli Tanga ambapo Agosti 5 atakutana na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents