Burudani

Foby: Ommy Dimpoz ni tofauti na wasanii wengine

Msanii wa muziki Foby amebainisha kuwa mkali kutoka lebo ya Rockstarr 4000 na boss wa PKP, Ommy Dimpoz ndio msanii pekee kwa upande wake ambaye yupo tofauti na wasanii wengine katika tasnia ya hiyo.


Foby

Akiongea na Bongo5 , Foby ameeleza kuwa Ommy amekuwa msanii anayefanya aina ya muziki  wa ainaa tofauti kuliko wasanii wengine  pia amekuwa akipangilia vyema maneno yake na meleody  vile vile mkali huyo wa ‘Ila’ amebainisha kuwa anafikiria kumuandikia ngoma msanii huyo.


Ommy Dimpoz

” Kuhusu kumwandikia Ommy Dimpoz, ngoma free ni kwa sababu ni mtu ambaye huwa anasema wazi halafu anathamini sana vitu vya wengine, mfano kusema nani kamwandikia na kwa kifupi namkubali tu,” amesema Foby.

Ameongeza ” Nimeanza kumkubali Ommy tangia enzi za ‘Nai Nai’, kabla hata sijatoka, niliona anafanya muziki wa pekee yake, ukimsikiliza ni tofauti na wasanii wengine kuanzia mpangilio wa maneno yake hadi melody.”

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents