Rais wa Brizil atoka hospitali

Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro ameruhusiwa kutoka Hospitali baada ya kuwepo hapo tangu siku ya Jumatano.

Bolsonaro, mwenye umri wa miaka 66 kwa siku 10 alikuwa akisumbuliwa na misuli ambayo hutenganisha kifua kutoka kwenye tumbo na ina jukumu muhimu katika kupumua [hiccups] na kulikuwa na wasiwasi juu ya afya ya kiongozi huyo tangu kuchomwa  na kisu tumboni wakati wa kampeni yake mnamo 2018.

Alijeruhiwa vibaya sana katika shambulio hilo na kupoteza 40% ya damu yake. Amekuwa akifanyiwa operesheni kadhaa tangu alipo patwa na tukio hilo.

Rais huyo wa Brazil aliwaambia waandishi wa habari kuwa anatarajia kurudi ofisini siku ya Jumatatu. Kulikuwa na hofu kuwa Bolsonaro anaweza kuhitaji kufanyiwa upasuaji ingawa jambo hilo lilikataliwa.

Related Articles

Back to top button