Siasa

Rais wa Marekani Joe Biden azungumza na Rais Kenyatta kwa simu (+ Video)

Rais wa Marekani Joe Biden amezungumzia mgogoro wa Tigray Ethiopia na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya. Mazungumzo hayo yamefanyika kwa njia ya simu siku ya Alhamisi, White House imeeleza.

Viongozi hao wawili wamejadili ” kuzorota kwa haki za binadamu na hali ya kibinadamu” jimboni Tigray.

Walizungumza kuhusu ”hitaji la kuzuia vifo na kuhakikisha misaada ya kibinadamu inawafikia”.

Tigray imekumbwa na mzozo tangu mwezi Novemba kati ya vikosi vya Ethiopia na vikosi washirika wa chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF).

Maelfu ya watu wanaripotiwa kuuawa, na karibu milioni mbili wamekimbia makazi yao.

Shirika la Msalaba Mwekundu mwaka huu limeonya kuwa uhitaji wa msaada wa kibinadamu ni ”mkubwa mno”.

Ikulu ya White House imesema kuwa Rais Biden amesisitiza kujitoa kwake kufanya kazi na Kenya kusaidia uimarishaji wa amani na usalama katika eneo hilo.

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CLywhILBYLP/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents