Siasa

Rais wa Tunisia amfukuza Waziri Mkuu na kusitisha Bunge kisa maandamano

Rais wa Tunisia amemfukuza kazi waziri mkuu kusitisha shughuli za bunge, kufuatia kuzuka kwa vurugu za maandamano katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana na kupambana na Polisi siku ya Jumapili kuonyesha hasira zao dhidi ya serikali kwa namna inavyoshughulika vibaya suala la Covid-19,

Rais Kais Saied alitangaza atasimamia hilo kwa kusaidiwa na waziri mkuu mpya, akisema anataka kuleta utulivu nchini humo. Lakini wapinzani wake wanasema hatua aliyoichukua Rais huyo ni kama kupindua ama mapinduzi ya kimamlaka.

“Tumechukua hatua hizi… mpaka hali ya Tunisia irejee kuwa shwari, mpaka tukiokoe nchi,” alisema Saied katika hotuba yake kwenye televisheni baada ya kuitisha kikao cha dharura cha usalama.

Usiku wa Jumapili, waandamamaji walilipuka kwa shangwe kufuatia taarifa kwamba waziri mkuu Hichem Mechichi ametimuliwa. Baadae Rais Saied akaungana na maelfu ya waandamamaji katika mji mkuu Tunis.

Maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana mjini Tunis na majiji mengine dhidi ya chama tawala wakipaza sauti sao kwa kusema “ondokeni!”, na kutoa wito wa bunge kuvunjwa.

Vikosi vya Usalama vilizuia maeneo ya Bunge na mitaa kadhaa karibu na eneo la Avenue Bourguiba, lililokuwa kitovu cha maandamano makubwa ya mwaka 2011 dhidi ya serikali yaliyoleta mapundudi makubwa nchini Tunisia.

Polisi walipiga mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji hao na kuwakamata watu kadhaa, huhu mapambano yakizuka baina yao katika miji kadhaa.

Waandamanaji walivamia maofisi ya chama tawala cha Ennahdha party, na kuharibu Kompyuta, na kuchoma moto kwenye ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho huko Touzeur.

Chama hicho kilikemea vitendo hivyo kikitupia lawama “vikundi cha wahalifu” waliokuwa wanajaribu kuleta “vurugu na kuleta taharuki “.

tunisia

Rais Saied aliapa kushughulikia vurugu zaidi zinazosababisha na vikosi vya usalama.

“Nawaonya yoyote anayefikiria kutumia silaha … na yeyote atakefyatua risasi,jeshi litajibu mapigo kwa risasi,” alisema.

Alisema katiba inamruhusu kusimamisha bunge kama kuna hatari. Lakini Spika wa bunge la Tunisia, Rached Ghannouchi amemtuhumu rais huyo “kukiuka katiba “.

“Tunaamini taasisi hizo zinaendelea na wafuasi wa Ennahda na watu wa Tunisia watalinda mapinduzi yoyote,” Ghannouchi, kiongozi wa chama cha Ennahda, aliliambia shirika la Reuters.

Miaka 10 iliyopita, mapinduzi ya Tunisi yalisababisha kuletwa kwa demokrasia na kuodnoa maasi katika eneo karibu lote la nchi za kiarabu.

Lakini matumaini kwamba mapinduzi hayo yangeleta ajira na fursa zingine yamekuwa tofauti.

Baada ya muongo mmoja, Tunisia inakabiliana na hali mbaya ya uchumi pamoja na athari mbaya za janga la corona.

Visa vimekuwa vikiongezeka hasa katika wiki za karibuni, na kuendelea kutishia zaidi uchumi wake unaodorora

Waziri mkuu Hichem Mechichi alimtimua waziri wa afya wiki iliyopita, lakini hatua hiyo haikusaidia sana kutuliza hasira za watu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents