Ray: Tunanyonywa lakini tusisahau tulikotoka


Msanii wa filamu nchini Vincent Kigosi aka Ray The Greatest amesema pamoja na kwamba bado wananyonywa na makampuni ya usambazaji wa filamu nchini, wasanii wa Tanzania hawapaswi kusahau walikotoka.
Ray amesema enzi wameanza uigizaji wa tamthilia zilizokuwa zikioneshwa ITV, walikuwa wakilipwa shilingi 40,000 ambazo zilikuwa zikigawanwa na wasanii wa kundi lote.
Amesema pamoja na kwamba hawapendi kuuza haki zao kwa wasambazaji ama makampuni ya ununuzi wa filamu zao, kutokuwepo kwa soko la uhakika ni jambo lisiloepukika japo tofauti na zamani leo hii wanamiliki makampuni na kumudu maisha yeo kwa kununua magari na vitu vingine.
Akiongea na mtandao wa Filamu Central Ray amesema serikali inatakiwa kuandaa mazingira yatakayoweza kushawishi wawekezaji wengi zaidi wanaoweza kuingia katika usambazaji wa filamu.
Jambo jingine alilopendekeza ni taasisi za kibenki kuwadhamini kwa kuwakopesha fedha kwa ajili ya kutengenezea filamu na kuziingiza sokoni ama kuuza nje ya nchi ili kuongeza maslahi na kuwafanya wasanii wasiuze haki zao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents