Burudani

Rayvanny awafunika Diamond Platnumz, Harmonize na Alikiba kwa hili, Atoa kauli hii

Msanii wa Muziki wa BongoFleva kutoka katika lebo ya WCB inayosimamiwa na Diamond Platnumz  @rayvanny, amefanikiwa Kufikisha zaidi ya Steams Milioni 15 kwenye Mtandao wa kusikiliza Muziki wa @boomplaymusic_tz, na kumfanya awe Mwanamuziki aliyesikilizwa zaidi kuliko wasanii wote Afrika Mashariki.

Kupitia Ukurasa wao wa Instagram, BoomPlay wamethibitisha hilo huku wakimpongeza  kwa kuwa Msanii wa Kwanza Kufikisha Streams zaidi ya Milion 15 katika Mtandao huo .

Kwa maana hiyo Rayvanny amewapita Diamond Platnumz, Alikiba, Harmonize, Eddy Kenzo na wengine ambao ni wasanii wakubwa kwa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Rayvanny ameandika ujumbe huu:-

“ONLY ONE ☝️ MSANII WA KWANZA KUFIKA 15M ( IWEKE KUMBUKUMBU ) Yani hapo Albamu bado iko ndani 😂😂😂 thanks alot @boomplaymusic_tz.      

So proud to be the Number one streamed artist on @boomplaymusic_tz Fan Love ❤️ !!!!! #CHUI 🐅🐅🐅. #WcbForLife 🔥🔥🔥🔥🔥

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents