Habari

RC Makonda akoshwa na upepo wa kisulisuli ‘Heri kelele za watu wanaomuomba Mungu kuliko za Bar’ (+video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda amewaomba viongozi wa Dini mbalimbali kwa imani zao, Watangaze Injili popote pale ndani ya mkoa huo bila wasiwasi wowote ule na serikali itawapa ushirikiano.

RC Makonda akiongea leo Jumatatu Oktoba 28, 2019 katika kongamano maalum lililoandaliwa kuelekea Uchaguzi, Uchumi wa viwanda, Amani, Mahusiano, Uzalendo na Ustawi wa Taifa, Amesema kuwa kuna watu wanaona kuomba usiku ni kama kupiga makelele lakini ni bora wanaopiga kelele za kumuomba Mungu kuliko kelele za Baa.

Kwa upande mwingine, RC Makonda amesema kuwa alikuwa hajui ‘Upepo wa Kisulisuli’ umeandikwa kwenye Quran huku akidadavua kuwa upepo huo kuna watu wanauelezea kwa maana zao lakini kiimani kuna watu unawaponya.

Kauli hiyo ya RC Makonda inakuja ikiwa wiki moja iliyopita DC Ilala, Sophia Mjema akaririwe na vyombo vya habari akisema siku za kusali ni tatu tu kwa wiki yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents