Michezo

Real Madrid wayaaga mashindano ya Copa del Rey kwa fedheha

Klabu ya Real Madrid imeyaaga mashindano ya kombe la mfalme nchini Hispania baada ya kukubali kichapo cha goli 2-1 dhidi ya vibonde Leganes.

Real Madrid wametolewa kwa faida ya magoli ya ugenini ambapo kwenye mchezo wa kwanza Madrid walishinda goli 1-0 ugenini kwahiyo jana wametolewa kwa kuruhusu goli 2-1  Santiago Bernabeu .
Matokeo mengine ya kombe hilo ni klabu ya Valencia dhidi ya Alaves ambapo Valencia walifungwa goli 2-1 Agregates (3-3) hata hivyo wamefuzu kwa changamoto ya penati 3-2 .

Hiki kinakuwa kipigo kingine cha fedheha kwa klabu hiyo ambapo kwa msimu huu Madrid wamepoteza mechi mbili uwanjani kwao Santiago Bernabeu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents