Burudani

Ripoti: AKA aligoma kupanda jukwaani kwenye utoaji tuzo ya Best International Act: Africa

Drama kwenye tuzo za BET ziliendelea tena mwaka huu. Kama kawaida, Wizkid alizipa mikausho mikali kwa si tu kwa kugoma kwenda kama wengine, bali hata kuzizungumzia kabisa. Lakini imebainika pia kuwa AKA na Yemi Alade walitoa mikausho yao. Yemi hakwenda kwenye utoaji wa tuzo katika vipengele vya Best International Act: Afrika na UK. Lakini AKA yeye anadaiwa kuwa alikuwepo ukumbini hapo lakini hakupanda jukwaani kama wengine.

Diamond, Cassper Nyovest na Black Coffie walikuwepo. Kutokana na kitendo hicho kumekuwepo na mjadala mkubwa Afrika Kusini kuwa AKA hakupenda ushindi wa Black Coffee ambaye wamewahi kutupiana vijembe kwenye Twitter kipindi cha nyuma. Hata Hivyo AKA amekanusha na amempongeza DJ huyo.

Screen+Shot+2016-06-26+at+11.15.11+AM

Screen+Shot+2016-06-26+at+11.15.28+AM

Screen+Shot+2016-06-26+at+11.15.20+AM

Hata hivyo AKA alihudhuria red carpet ya show yenyewe.

13473345_991094524343856_1767022521_n

Cl7tTbSUYAQnJCN.jpg_large
AKA na girlfriend wake, Bonang Matheba

Katika hatua nyingine, Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amempongeza Black kwa ushindi wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents