Burudani

Rita Paulsen asimulia jinsi alivyopuuzwa wakati anaanzisha Bongo Star Search (Audio)

Miaka 10 iliyopita, Rita Paulsen alikuwa ni mwajiriwa aliyetoka kufukuzwa kazi ITV na kuanzisha kampuni yake ya Benchmark Productions akiwa na miaka takriba 23 tu.

11378001_847457125337957_2100279981_n

Kampuni hiyo ndio ikatengeneza njia ya video za muziki za wasanii wa Bongo Flava kwa kuongoza pamoja na zingine, video ya Machozi ya Lady Jaydee na Zali la Manteli ya Professor Jay.

Kichwani kwake alikuwa na wazo kubwa ambalo kwa wengi lilionekana kama kwenda mwezini.

“Nilivyokuwa naongelea hilo suala (Bongo Star Search), na watu waliokuwa karibu na mimi wakaniambia ‘you are crazy, hiyo show ni ya milioni sijui ngapi za dola, huwezi kufanya, kwanza watu hawawezi kujitokeza,’ Rita alikiambia kipindi cha Chill na Sky.

Rita anasema baada ya kukatishwa tamaa, wazo hilo aliliweka pembeni kidogo kwa miaka mitatu lakini aliamua kuisajili kwanza.

“Sikuweza kuifanya kwasababu niligundua inahitaji fedha nyingi, sio nyingi sana lakini nilikuwa nimeshakatishwa tamaa,” anakumbuka Madam Rita.

Hata hivyo ongezeko la wasanii waliokuwa na kipaji lakini hawana uwezo na waliomsumbua awasaidie ilizidi kumsukuma zaidi kulifanyia kazi wazo hilo.

“Tukawa tunafanya kazi zingine, tukafanya kazi moja ya wizara ya afya wakatupa hela nzuri nikasema ‘this time I am going to do Bongo Star Search.’

Mara ya kwanza aliamua kufanya Bongo Star Search Dar es Salaam peke yake. Anakumbuka kuwa kutokana na bajeti ndogo waliyokuwa nayo, walifanya matangazo kwa kiasi kidogo tu kuhusiana na usaili ambao ulifanyika Bilicanas.

“Nakumbuka mtu wa kwanza niliyetengeneza naye jingle ya kupromote Bongo Star Search alikuwa ni AY. AY alikuwa mdogo sana, alikuwa hajakuwa star kwahiyo alikuwa kila siku yupo ofisini kwetu.”

Anasema siku ya usaili aliamini kuwa mahudhurio yangekuwa machache mno lakini kwakuwa alikuwa ameyavulia maji ilimlazimu kuyaoga.

“It’s like nobody believed in the idea kwasababu tulijaribu kuuza for three years on paper kila mtu alikuwa anatuambia ‘tutawatafuta.’
Tulisema watu wafike saa 12 saa moja. Mimi nikatoka nyumbani naendesha gari, nimefika Bilicanas ilikuwa kama saa nusu, karibu nipate ajali! Sikutegemea, watu walikuwa wamepanga mstari kutoka Bilicanas mpaka Posta, mpaka Daily News kule, that’s how bad I was. Nikatamani nirudi nyumbani, ‘we can’t, tutaanzia wapi.’

Madam Rita anasema usaili huo ulifanyika kwa siku tatu na mtu wa kwanza kufika alikuwa ni Jumanne Idd aliyefika saa 10 alfajiri na ndiye alikuwa mshindi.

“It wasn’t easy,” anasema Madam.

Shindano hilo lililofanyika kwa miaka minane sasa limerejea tena na mwaka huu usaili utafanyika katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents