Burudani

Usiogope kutoa wimbo wa ‘kinyamwezi’, kama ni mzuri mashabiki wataupenda tu – Vanessa Mdee

Vanessa Mdee amesema Closer na Nobody But Me ni nyimbo zilizomfanya aelewe kuwa mashabiki wa muziki Tanzania hawana aina moja ya muziki wanaoupenda.

Nominee huyo wa tuzo za MTV MAMA mwaka huu, ameiambia Bongo5 kuwa kama wimbo ni mzuri hata ukiwa na ladha ya Kimarekani watu wataupenda tu.

“Nadhani mapokezi ya muziki Tanzania siku hizi yameanza kubadilika,” amesema.

“Masikio ya wananchi na mashabiki wa muziki mzuri yanazidi kupanuka na watu wanakubali vitu tofauti kutoka kwa wasanii wa Tanzania wa kizazi kipya. So tumeacha tumekariri na nadhani ni ujumbe wangu kwa wale wanaotengeneza muziki, waache kukariri.There is no correct formula, niamini hakuna hata njia mtu anaisema kwamba nifanye hivi na hivi,” ameongeza.

“Nitakupa mfano, kuna kipindi Cpwaa alitoa nyimbo fulani inaitwa Problem.. it was a big song. Nyimbo ilikuwa ya kinyawezi yaani shout outs to Lucci, it was such a big song. Mpaka leo watu wanaikumbuka hiyo nyimbo na sio eti sasa hivi, it’s an old song but it’s massive. Huo ni mfano wa kwamba bado wapo watu wasikiliza wa muziki mzuri so tusikariri.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents