Promotion

Road to MAMA party kufanyika Kesho Dar

Wasanii Diamond na Joh Makini kutoka Tanzania,Wande Coal (Nigeria), Moze Radio na Weezle  ( Uganda) pamoja na P unit(Kenya) na Ma Dj Code Red kutoka Kenya Ijumaa ya kesho watakamua vilivyo pale Club Maisha

katika ile party maalum ya kuelekea katika fainali za tuzo za muziki za MaMa “Road To Mama Dar-Es-Salaam Party” zinazoandaliwa na kituo cha televisheni MTV Base, tuzo ambazo zinatarajia kufanyika tarehe 11 December jijini Lagos nchini Nigeria.

Road To Mama party ni mwendelezo wa Pati  za kuelekea kwenye Tuzo hizo ambapo wiki iliyopita party ya kwanza ilifanyika jijini Kinshasa nchini DRC Congo na sasa party hiyo imehamia Dar-Es-Salaam katika ukumbi wa burudani  Club Maisha.

Akiongea katika utambulisho wa wasanii ha leo mchana katika hoteli ya Kempinski jijini DSM mwakilishi wa MTV Base Tanzania, Seven Mosha, aliwataja Diamond, P Unit, Wande Coal pamoja na Code Red, ambao pia walikuwepo katika shughuli ya utambulisho huo kwa waandishi wa habari, alielezea kuwa Joh makini na Moze Radio watakuwepo siku ya kesho usiku.

Naye meneja wa masoko wa kampuni ya Airtel bwana Kelvin Twissa alichukua nafasi hiyo kuongelea mchango wa kampuni yake kama wadhamini wakuu wa tuzo hizo na kusema kampuni ya Airtel itaendelea kushirikiana na Mtv Base pamoja na wasanii kutoa burudani nzuri katika tasnia ya muziki kwa kuwa tuzo hizo ni maarufu na kubwa pamoja na kuwa na umuhimu mkubwa barani Afrika.

Bwana Twissa alichukua nafasi hiyo kutaja vyombo vya habari ambavyo vimepata nafasi ya kulipiwa gharama zote na Kampuni ya Airtel ili kuripoti tukio hilo la Tuzo za MaMa kule Lagos Jijini Nigeria. Alivitaja vyombo hivyo vya habari kuwa Gazeti la Citizen na Championi, Clouds Radio na Radio One.

Nao wasanii wakizungumza na waandishi wa habari walisema wanashukuru wadau mbali mbali ambao wamekuwa wakijitokeza kwa nyakati mbali mbali kuwapa sapoti kama walivyofanya Airtel kwa namna ambavyo wanachangia wasanii na muziki kufika mbali zaidi ikiwemo kubadilishana mawazo kati ya wasanii na wasanii.

Wasanii hao wakiongozwa na Diamond, Code Red Djs pamoja na P unit waliwaomba wapenzi, mashabiki na wadau wa muziki wa Tanzania na Kenya kuwapigia kura katika mchakato huo wa Tuzo pamoja na kujitokeza kwa wingi kesho kujimwaya mwaya kwenye party hiyo.

Kumpigia kura Diamond kwa kutumia simu yako nenda kwenye kiboksi cha meseji na andika BNA weka nafasi andika DIAMOND alafu tuma kwenda namba 6262

Kumpigia kura Diamond kwa kutumia simu yako nenda kwenye kiboksi cha meseji na andika BNA weka nafasi andika DIAMOND alafu tuma kwenda namba 6262

Kuwapigia kura P UNIT andika PUnit – Kare (Kenya) BG P UNIT TO alafu tuma kwenda namba 6262

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents